about_header

MCHANGO


Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010 Mobisol imefunga zaidi ya mitambo 60,000 ya sola kwa wateja wake katika miradi mitatu (3) ya majaribio Tanzania, Rwanda na Kenya. Wateja wetu wanatoa mrejesho chanya na wanaelezea ni kwa jinsi gani ubora wa maisha yao ulivyoboreshwa tangu walipomilikishwa mitambo yao ya sola za nyumbani za Mobisol. Hayo yote yanathibitisha mafanikio na uakisi wa muundo bora wa biashara ya Mobisol.


Mobisol-technicians-300x184

Mobisol inatoa nishati safi na salama kwa maelfu ya jamii za vijijini zisizo na nishati ya uhakika.

Kwa kumiliki mitambo ya nyumbani ya sola wanajamii wa kipato cha chini wanapata nishati sahihi hivyo kusaidia kuinua kiwango cha ubora wa maisha yao kwani ni jambo muhimu kwao. Watumiaji wa mitambo ya sola za Mobisol hawana haja tena ya kutegemea mafuta ya taa kwa kwa kupata mwanga wala hawahitaji genereta kwa kuwezesha matumizi ya vifaa vyao. Na sasa wako huru na soko gumu la nishati pamoja na mfumuko wa bei za nishati nyingine tofauti na sola za Mobisol.

Nishati inayopatikana katika mtambo wa sola za Mobisol kimsingi inawagharimu wateja  kiasi kidogo cha fedha kulinganisha na hapo nyuma walipokuwa na matumizi ya huduma za nishati kama mafuta ya taa, mishumaa na betri za magari. Hewa chafu iliyokuwa wakati wote ndani ya nyumba itokanayo na vibatari na kelele za jenereta za dizeli zimeondolewa kwa utambulisho wa nishati safi,tulivu na salama ya sola za Mobisol inayohakikisha usalama wa afya na utulivu zaidi katika mazingira ya kazi ya wateja.


boy-studying-with-solar-lantern02-300x184

Upatikanaji wa nishati unaleta mafanikio ya kijamii na kiuchumi.

Upatikanaji wa taa za teknolojia ya LED zinatoa mwangaza bora na mzuri kuliko wa vibatari. Kwa kupitia wanawake na watoto inathibitishwa ya kwamba  watu wanahisi usalama wa maisha yao umeongezeka tangu walivyoweza kumiliki mtambo ya sola kutokana na  muda mrefu  wa mapumziko nyakati za usiku.

Nyongeza ya hayo, kutokana na ongezeko la masaa yenye mwanga, wateja wanaweza kujihusisha na shughuli za kimaendeleo hadi nyakati za usiku na pia mapema katika masaa ya  asubuhi. Idadi kubwa ya wateja wa Mobisol wameelezea furaha yao juu ya maendeleo mazuri ya kielimu ya watoto wao kutokana na kupata muda wa ziada wa  kujisomea usiku. Wateja wengine kwa mfano wametumia muda huu wa ziada ulioongezeka kutokana na sola kwa kufanya kazi katika karakana, maduka na hata wengine kushona nyakati za usiku.


mobicharger-shop02-300x184

Wateja wajasiriamali wanawezeshwa kuanzisha biashara zao wenyewe.

Takwimu zinaonyesha robo tatu ya weteja wa Mobisol walio nje ya gridi ya taifa ya umeme wameanzisha biashara ya kuuza ziada ya nishati wanayoizalisha kila siku. Mobisol inapongeza na kutia hamasa kwa muamko huu kwa mpango wetu wa “biashara nje ya sanduku” ambao unalengo la kumuwezesha mteja kuwa na namna nyingine za kujiongezea kipato kama kutoa huduma za kunyoa nywele, kituo cha kuchaji simu na tochi. Na kwa huduma yetu kubwa ya kuwasha jokofu wateja wa Mobisol wanaweza kufurahia vinywaji baridi na kuhifadhi mazao ya shamba au madawa.
capacity-building-300x184

Mobisol inafanikisha uwezeshaji pamoja na ajira katika jamii za vijijini.

Mafunzo na ajira kwa mafundi wazawa na maafisa masoko vijijini inatoa nafasi za ajira katika mikoa yenye idadi kubwa ya watu wenye ukosefu wa ajira. Pia Mobisol inahimiza usawa katika jinsia kwa kuajiri na kutoa nafasi kwa za ajira kwa wanawake. Mobisol inaongeza ubora wa maisha katika jamii za vijijini na hivyo kupunguza ongezeko la watu mijini hivyo kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
house-with-panel-300x184

Mitambo bora kabisa ya sola ya nyumbani ya Mobisol inafaida kubwa katika mazingira.

Mitambo nafuu na ya teknolojia ya juu  ya Mobisol inatoa nafasi kwa mteja kumiliki mtambo bora utakaodumu kwa muda mrefu na uliosahihi kwa mahitaji ya umeme. Uvunaji wa nishati ya jua unachochea afya bora kwa watu na sayari nzima tuliyopo, kimsingi nishati ya sola ni bora zaidi katika kufanikisha hayo. Upatikanaji wa nishati mbadala na maendeleo makubwa ya teknolojia ya sola duniani itachangia moja kwa moja katika kupunguza ongezeko la hewa ya ukaa duniani.
vision2015-300x184

Maisha ya baadae yanaonekana angavu kwa nishati ya sola barani Africa.

Matokeo chanya yaliyojumuishwa kotoka katika miradi ya majaribio ya mobisol yamepelekea mpango wa ufungaji wa mitambo 60,000 kwa nchi za Tanzania, Rwanda, na Kenya kwa mwaka 2016. Kwa miaka ijayo, Mobisol inadhamiria kuwafikishia huduma mamilioni ya wateja wa kipato cha chini ili kusaidia kuwainua kiuchumi na kijamii na katika nchi zilizo katika miradi hii kwa pamoja iatasaidia katika kutunza mazingira.


Angalia filamu ya Mobisol:
Jifunze zaidi kuhusu: Chuo cha Mobisol.