Akademie_header_jumping!

KITUO CHA MAFUNZO CHA MOBISOL


Ni vipi tunapata watu wenye utaalamu  katika teknolojia  ya sola?”

Hili lilikuwa changamoto kubwa Mobisol iliyokumbana nayo  wakati wa ukuwaji wake. Suluhisho letu: kituo cha mafunzo cha Mobisol!

Technical training at the Akademie

Kituo hiki ni taasisi ya mafunzo kwa wajasiriamali wazawa,wahandisi wa Mobisol na wafanyakazi. Madhumuni ya kuanzishwa kwa kituo hiki cha mafunzo ni kuwapa mafunzo na kuwawezesha wajasiriamali kufanya kazi kama mafundi wa Mobisol na maafisa mauzo kwa kutumia elimu ya kiwango husika kufanikisha huduma kwa wateja na kuiwakilisha Mobisol kama kiongozi katika utoaji wa nishati endelevu afrika mashariki. Mafunzo ya zingatia viwango vya juu vya kimataifa vya masoko na elimu ya ufundi na inatolewa kwa umakini na jopo la mafundi wazawa waliochaguliwa na kupatiwa elimu sahihi.

Misingi ya kitaalamu ni sababu zilizopelekea kuhakikisha wafanyakazi wa Mobisol wanatoa bora, elimu na pia wakikidhi viwango vya usalama na tahadhari wakati wa ufungaji wa mitambo. Ni timu ya mafundi walio na hamasa, kujitolea na wenye mafunzo sahihi tu, kutoka katika timu huru ya wakilishi wa mauzo mpka katika ngazi ya uongozi wanathibitisha ufanisi wa mtiririko wa kazi, huduma bora kwa wateja na pia kwa kiasi kikubwa muundo bora na endelevu wa umeme.


Mobisol training systems

Elimu bora na eneo salama la kazi.

Mapema mwaka 2014, muda mfupi baada ya soko kuingia Rwanda, kituo cha mafunzo cha mobisol Nyamata, Rwanda kilianzishwa na baadae mwezi mei 2014 kituo cha pili cha mafunzo kiliasisiwa Arusha, Tanzania. Kwa baadae vituo vingine vya kutoa elimu vitafunguliwa katika miradi mingine itakayofunguliwa katika nchi zingine ili kutoa nafasi kwa kila eneo kupata elimu bora na kukidhi hitaji la kutoa huduma bora zinazohitajika katika viwango vya Mobisol.

Vipindi vya mafunzo katika kituo cha elimu vinatolewa kwa wawkilishi binafsi wa mauzo na mafundi wa sola ambao kwa sasa wameajiriwa na Mobisol na wanaendelea kupata nafasi za kujielimisha zaidi kiujuzi kwa malengo ya kupata nafasi za juu zaidi za ajira.


Mafunzo kwa wajasiriamali binafsi katika taaluma ya teknolojia ya sola na masoko.

Wajasiriamali binafsi waliojiajiri na wenye mipango ya kufanya kazi ya wawakilishi wa mauzoau mafundi wa sola wa Mobisol  wanapata mafunzo ya hali ya juu kabisa ya wiki mbili katika kituo cha mafunzo cha Mobisol. Wanafunzi wote wanapewa elimu ya msingi endelevu  ya Mobisol katika Nyanja ya umeme na baadae wakielekea katika moduli ya elimu kwa vitendo. Mafunzo ya ziada yanafanyika kwa kupitia utendaji wa kimajaribio ambao umpata uzoefu mwanafunzi kupata ujuzi kutatua matatizo ya mara kwa mara yanayojitokeza katika maeneo ya kazi. Wanapomaliza mafunzo kwa nadharia wanafunzi wanaelekezwa katika mafunzo kwa vitendo kwa undani na umakini zaidi. Na pale wanapomaliza mafunzo yao kwa vitendo na kufaulu mitihani, mafundi na wawakilishi wa mauzo wanatunukiwa vyeti na kuhakikishiwa ajira ya mkataba huru na Mobisol.

Vyeti vinavyotunukiwa vinapewa uhalali wa kimatumizi wa miezi sita tu. Na baada ya hapo anaweza kupata mafunzo kwa ajili ya kuthibitishwa kwa kupata cheti kingine cha miezi sita mbeleni. Kwa utaratibu huu una hakikisha elimu inakuwa ya kisasa zaidi na ina hakikisha wahitimu wa kituo cha mafunzo wanaendelea na kupata taarifa kuhusu teknolojia mpya zinazoendelea kuingia na maendeleo ya huduma.


Mafunzo ya nafasi za usimamizi na ualimu.

Kituo cha mafunzo cha Mobisol kinatoa mafunzo yanayofuatana yanayotoa elimu juu ya nafasi ya uendeshaji wa masoko (wasimamizi wa usambazaji& na vituo vya mauzo), mafundi wa ukarabati na watoa huduma kwa wateja.nyongeza ya hayo kuna nafasi za masomo zinazotolewa kwa wafanyakazi wa mobisol kwa mfano kuongoza elimu na maarifa katika michakato ya usimamizi, kuwa waelekezi katika kituo cha mafunzo cha mobisol na pia kuhudhuria mafunzo ya lugha pamoja na masuala ya uwekaji kumbukumbu na mafunzo ya dijitali ya taarifa.

Mafunzo yanayotolewa na mafundi wazawa waliofuzu waliopata mafunzo maalumu na ambao tayari wana uzoefu wa kufundisha au pia wanautaalamu na uzoefu kama wafanyakazi wa Mobisol.

Mtaala unaandaliwa na kuboreshwa na uongozi wa Mobisol uliopo ujerumani na unapewa nguvu zaidi na wasimamizi wazawa kutoka afrika. Timu zote kutoka kila nchi zinatoa muongozo katika kuboresha moduli za vitendo. Na ndio hapo panapopatikana utajiri mkubwa wa uzoefu  kwa watumishi wetu wa ndani na shughuli zao za kila siku katika kazi zinakuwa ndani ya mkakati huu. Katika kila nchi yenye mradi mwendeshaji wa eneo husika la mafunzo anakuwepo na anahusika kwa kupanga,kuongoza na pia kuwasiliana na timu ya ujerumani.


Kuenea kwa maarifa na uwezeshwaji  vijijini.

Mafundi wa sola na mawakala wa mauzo ni wajasiriamali wanaofanya kazi zao wenyewe katika vijiji vya husika na baada ya maeneo ya miji katika vituo vya mauzo(tawi la soko) na mengi katika matawi hayo tayari yana mizizi madhubuti katika mikoa yao na jitihada zinakuwa ndogo katika kupeleka elimu mpya ya teknolojia ya sola, utangazaji wa bidhaa za Mobisol na na taarifa moja kwa moja katika jamii zao.

Kwa sasa, wanafunzi 20 wanapata mafunzo kila baada ya wiki mbili na jitihada zinafanyika kuhakikisha usawa kati ya wanawake na wanaume.kwa kutoa mafunzo kwa vijana wa vijijini katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara vyuo vya mafunzo vya Mobisol pia vinatoa mchango mkubwa sana katika kuziwezesha jamii za vijijini. Mafunzo ya kitaalamu na ya vitendo pia yanatoa utalaamu na utendaji mzuri kwa kwa wazawa kwa rasilimali kwa usahihi na kuleta “maendeleo” kwa mikono yao wenyewe.

Uzinduzi wa Kituo cha Mafunzo Cha Mobisol Tanzania.Angalia filamu ya Mobisol Akademie: