Mobisol80WpSHS_MobisolTZ

BIDHAA


Mobisol easy installation

Mtambo wa sola wa nyumbani unaotolewa na Mobisol upo tayari kwa matumizi na ni rahisi kwa ufungaji.

Mitambo ya mobisol inapatikana katika aina tofauti tatu kuannzia mtambo wa wati 80, 120 mpaka wati 200. Mitambo hii bora kabisa ya sola za majumbani inabuniwa na kusanifiwa Ujerumani kwa lengo la kukidhi ufanisi, kuzalisha mwanga bora na kupata mitambo iliyorahisi kwa mahitaji ya nyumbani na biashara ndogondogo. Mitambo hii inapatikana ikiwa kamili kimatumizi ikiwa pamoja na taa za kumulika, tochi, chaja ya simu na baadhi ya vifaa muhimu vya kukamilisha mtambo ikiwa ni pamoja na nyaya na kifaa cha kuwashia taa na vinginevyo.

Mitambo ya mobisol inayoendeshwa kidigitali inafungwa kirahisi na mafundi wazawa waliopata mafunzo sahihi na ya kisasa kutoka chuo cha Mobisol. Katika hali ya urahisi kabisa mtambo unaweza kufungwa kwa zana kama nyundo.


Microfinance vis SMS

Taratibu zetu za kimauzo zinarahisisha bidhaa ya sola yenye ubora wa juu kabisa kupatikana kwa unafuu mkubwa.

Utaratibu wa malipo ya awamu mteja anaendelea na matumizi ya mtambo yanampa ahueni mteja asiye na uwezo wa kununua mtambo kwa mara moja kuweza kumiliki mtambo bora kabisa na kupata urahisi katika ulipaji. Matumizi ya simu katika huduma za kibenki kama M-PESA pamoja na mpango wa malipo ya mtambo wa sola mwa miezi 36 wa malipo ya awamu unaotolewa na Mobisol, inamuwezesha mteja kulipa kwa utulivu na mahali popote alipo.


Mobisol Tanzanian technican

Huduma bora baada ya mauzo zinazohakikisha ufanisi wa muda mrefu wa mtambo.

Mtambo wa sola wa majumbani wa mobisol unakuja moja kwa moja na waranti (uhakika wa kukidhi ufanisi) ya miaka mitatu (3) kwa betri na  miaka ishirini (20) kwa kifaa cha kuvunia mionzi ya jua (paneli). Tofauti kabisa na bidhaa nyingine za sola zilizopo sokono, bidhaa za sola za Mobisol zinafungwa pamoja na mpango kabambe wa huduma kwa mteja.

Kwa kutumia kifaa maalum cha kidigitali cha mawasiliano ndani ya kiendeshi cha sola,taarifa za kitaalamu kutoka katika paneli zinapatikana na kuhifadhiwa katika hifadhi maalumu na salama katika mtandao. Teknolojia hii inayoendeshwa kitaalamu inasaidia kutoa huduma muhimu na kutoa taarifa sahihi. Timu yetu ya wataalamu na mafundi inatoa huduma bure kwa wateja na ukarabati wa mitambo wakati wote wa waranti ili kuhakiki matumizi bora na ya muda mrefu ya mtambo husika. Huduma ya bure ya mawasiliano kati ya wateja na Mobisol pia inapatikana.
Jifunze zaidi kuhusu bidhaa zetu:

80w_Package

Mtambo wa wati 80

Mtambo wa wati 80 unatoa umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya nyumbani ya kiwango cha kati, mtambo huu una uwezo wa kuwasha taa saba (7) kuchaji simu za aina tofauti, redio, kuwasha runinga kwa masaa kadhaa ndani ya siku, kwa namna nyingine mtambo huu wa nyumbani wa sola unaweza kuhudumia nyumba ndogo au duka na pia kutoa huduma ya kuchaji simu ili kujipatia kipato cha ziada.

120w_Package

Mtambo wa wati 120

Mtambo huu wa sola unatoa umeme wa kutosha, unaweza kuhudumia nyumba ya ukubwa wa kati kwa kuwasha taa saba (7) na matumizi ya burudani mbalimbali kama kuwasha runinga, compiuta mpakato (laptop),redio na sanuri za kidigitali. Lakini pia, unaweza kuutumia kuhudumia nyumba ndogo au duka kwa mfano, kuchaji simu za mkononi au huduma ya kunyoa nywele kwa kujiongezea kipato cha ziada.

200w_Package

Mtambo wa wati 200

Mtambo wa wati 200 unatoa umeme wa kutosha mfano, una uwezo wa kuhudumia nyumba kubwa kwa kuwasha taa ishirini (20) na wakati huo huo kuwasha runinga, kuchaji simu kadhaa na pia kuwasha jokofu la sola.
Pia, unaweza kufanya matumizi makubwa ya burudani mbali na kuangaza nyumba. Mtambo huu ni sahihi kwa kuhudumia biashara mbili kwa wakati mmoja kama huduma ya kunyoa nywele na kifaa cha kuchaji simu.

Mobisol Suluhisho la Biashara

“Biashara nje ya sanduku” ya mobisol imejumuisha mtambo wa wati 80 na 200 ya Mobisol ambayo pia ni mitambo ya nyumbani, katika kila kifaa kuna vitu vyote muhimu sambamba na kabrasha za mafunzo zinazotoa msaada wa kuanzisha biashara kama kitabu cha vielelezo na makala za taratibu za kifedha. Vifaa vya kibiashara vinatolewa na visaidizi vya utangazaji wa biashara kama kadi za punguzo, kadi za wateja na bango la kutundika mbele ya duka.


Mobicharger

Chaja ya sola

Chaja ya sola “biashara nje ya sanduku” inapatikana pamoja vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kuanzisha biashara ya kuchaji simu. Ina sehemu tofauti tofauti za kuchaji simu za aina tofauti kumi na vifaa vingine kama tochi na vifaa vinavyotumia waya unganisha wa mawasiliano (USB) na pia kwa mwenye waya unganisha anaweza kuchaji simu ya aina yeyote.


sola_kinyosi

Sola kinyozi

Kifurushi cha sola kinyozi kinapatikana kikiwa na vifaa vya kuanzia huduma ya kunyoa nywele kama mashine ya umeme ya kunyolea nywele, vitana, vitana vya kuweka mitindo mbalimbali ya nywele pamoja na kifaa cha kusafishia.

Jifunze kuhusu: Mchango wa bidhaa zetu.