about_header

Mobisol


Mobisol – inaangaza dunia!

Mobisol inajumuisha nishati ya sola na mpango rahisi wa malipo kupitia simu za mkononi. Huduma bora kwa wateja na njia salama za usimamizi wa teknolojia.

Kampuni hii yenye makao makuu yake Ujerumani inawasaidia watu wa kipato cha chini kupata huduma za sola za kiwango cha juu kabisa. Nishati ya sola kutoka Mobisol ni safi na salama kwa afya ya binadamu na ni mbadala wa nishati nyingine zilizo na madhara kwa binaadamu na mazingira na pia ni za gharama za juu zaidi.

Mitambo yetu inakuja kwa ukubwa tofauti kulingana na mahitaji ya mteja, kuanzia wati 80 hadi wati 200 kukidhi mahitaji mbalimbali ya nyumbani. Mitambo ya sola ya nyumbani ina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kuwaasha taa, redio, kuchaji simu, na matumizi mengine ya nyumbani na shughuli nyingine za wateja. Mitambo yetu mikubwa inauwezo wa kuzalisha nishati kwa biashara ndogo zinazoweza kumuongezea mteja mjasiriamali kipato cha ziada.

Kwa namna hiyo basi, Mobisol inakuwa ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania na pia inachangia jitihada za dunia za kulinda mazingira.


Angalia Filamu ya Mobisol tukisherekea ufungaji wa mitambo ya sola elfu ishirini (20,000):